Waziri wa Afya azindua mradi wa TUWATUMIE Itilima mkoani Simiyu - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waziri wa Afya azindua mradi wa TUWATUMIE Itilima mkoani Simiyu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amezindua rasmi mradi wa TUWATUMIE unaotekelezwa katika wilaya za Itilima mkoani Simiyu na Misungwi mkoani Mwanza. 
 Uzinduzi wa mradi huo unaotekelezwa na shirika la Amref Health Africa Tanzania pamoja na taasisi ya Benjamin Mkapa umefanyika katika wilaya ya Itilima, ukilenga kuboresha huduma za afya hususani huduma za uzazi ili kupunguza vifo vya akina mama na watoto chini ya miaka mitano. 
 Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Waziri Mwalimu amesema serikali itaendelea kuboresha huduma za afya ikiwemo kuongeza watumishi wa afya pamoja na kuwatumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii ili wasaidia kutoa huduma za afya kwa wananchi. Naye Mkuu wa Miradi kutoka shirika la Amref Health Africa Tanzania, Dkt.Aisa Muya amesema utekelezaji wa mradi wa TUWATUMIE unaofadhiliwa na serikali ya Ireland kupitia shirika la Irish Aid, ulianza mwezi Disemba 2017 na unatarajiwa kufikia tamati mwezi Juni mwaka 2020 ambapo ametoa rai... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More