WAZIRI WA FEDHA DKT MPANGO AIPONGEZA BENKI YA AMANA KWA KUTOA HUDUMA BORA KWA JAMII - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI WA FEDHA DKT MPANGO AIPONGEZA BENKI YA AMANA KWA KUTOA HUDUMA BORA KWA JAMII

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Tanga

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewataka wakazi wa mkoa wa Tanga kutumia fursa ya uwepo wa Amana Benki katika mkoa huo kama fursa ya kujipatia Maendeleo kutokana na benki hiyo kuwa na huduma ya mikopo isiyokuwa na riba.

Waziri Mpango amesema hayo mkoani Tanga wakati alipokuwa akimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo katika mkoa huo."nimefurahishwa na jitihada za Amana Bank katika kutanua huduma zake kwa wananchi wa mikoani. Vilevile, nimewasisitiza wana Tanga kutumia fursa waliyopata kutoka Amana Bank kwa kuwafikishia huduma za bank hiyo kwao,ikiwemo mikopo bila riba jambo ambalo litawasaidia sana kujiinua kichumi kwa kukopa na kurejesha kwa wakati"amesema Waziri Mpango.

Akizungumza kwa niaba ya benki hiyo Mkurugenzi wa Amana Benki Dk Muhsin Masoud, amesema Benki ya Kiislamu ya Amana hapa nchini imefungua tawi lake jipya jijini Tanga ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Benki hi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More