Waziri wa fedha Kenya Henry Rotich akamatwa baada ya kujisalimisha kuhusu tuhuma za ufisadi - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waziri wa fedha Kenya Henry Rotich akamatwa baada ya kujisalimisha kuhusu tuhuma za ufisadi

Waziri wa fedha Kenya Henry Rotich amejisalimisha kwa maafisa wa upelelezi hii leo, muda mfupi baada ya mkurugenzi wa mashtaka nchini kuagizwa akamatwe.Kwa mujibu wa Nairobi News, Waziri Rotich alipelekwa kwa gari hadi katika makao makuu ya idara ya upelelezi ambako anahojiwa kuhusu malipo yaliotolewa kwa ujenzi wa mabwawa mawili nchini.


Anatuhumiwa kukiuka muongozo wa utoaji wa kandarasi iliopewa kampuni ya Italia CMC de Ravenna yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 450 kwa ujenzi wa mabwawa.


Kwa mujibu wa BBC.Hapo awali, mkurugenzi wa mashtaka Kenya aliagiza kukamatwa kwa waziri wa fedha Henry Rotich na ashtakiwe kuhusu ufisadi


Mkurugenzi huyo wa mashtaka Noordin Haji amekuwa akizungumza katika vyombo vya habari kuhusu uamuzi wa kumshtaki waziri wa fedha Kenya Henry Rotich, na maafisa wengine wa serikali kuhusu kandarasi zilizotolewa kwa kampuni ya Italia kujenga mabwawa mawili.


Noordin Haji ameeleza kwamba watashtakiwa kwa “kupanga kufanya udanganyifu, kushindwa kutii muongozo ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More