WAZIRI WA KILIMO AAGIZA KURUDIWA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA USHIRIKA KILA MAHALI PENYE DOSARI WILAYANI IKUNGI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI WA KILIMO AAGIZA KURUDIWA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA USHIRIKA KILA MAHALI PENYE DOSARI WILAYANI IKUNGI

Na Mathias Canal-WK, Singida

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Afisa ushirika wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Ndg Gurisha Msemo kufanya ziara ya kikazi maeneo yote kuliko fanyika uchaguzi wa viongozi wa vyama vya ushirika ili kubaini uhalali wa uwepo wao.

Mhe Tizeba ametoa kauli hiyo mara baada ya wakazi wa Kijiji cha Mkunguakihendo na Misughaa Wilayani Ikungi kuonyesha kutotambua namna walivyochaguliwa viongozi waliopo madarakani kukiongoza chama hicho katika ngazi mbalimbali jambo ambalo lina ashiria kupatikana kwa viongozi hao kinyume na utaratibu.

Dkt Tizeba ameyasema hayo jana 8 Juni 2018 wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika vijiji hivyo ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida.“Pamoja na maelekezo yangu ya kutazamwa mahali penye matatizo na kufanyika upya uchaguzi lakini pia nawasihi pindi utakapofanyika uchaguzi mchague viongozi waadilifu ambao watawasimamia katika kweli na haki... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More