WAZIRI WA KILIMO AAGIZA VYUO VIKUU KUTANGAZA MATOKEO YA TAFITI ZAO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI WA KILIMO AAGIZA VYUO VIKUU KUTANGAZA MATOKEO YA TAFITI ZAO

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Kilimanjaro
Imebainika kuwa tafiti na machapisho mengi yanayofanywa na wanataaluma na wanafunzi katika Vyuo mbalimbali si tu zinasaidia kujenga taswira za vyuo bali zinapaswa kuwa sehemu ya kufanya elimu iwe nzuri na bora zaidi.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 6 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye sherehe ya nne ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Mhe Hasunga amewaagiza watendaji wa Chuo hicho sambamba na vyuo vingine nchini kufanya tafiti za kutosha katika tasnia ya ushirika na kuhakikisha kuwa Matokeo ya tafiti hizo yanawafikia walengwa. "Serikali nayo kwa upande wake imeweka na itaendelea kuweka mazingira rafiki zaidi yatakayosaidia kuimarisha dhana ya ushirika miongoni mwa jamii ya watanzania" Alisema
Alisisitiza kuwa moja ya kadhia inayovikumba vyuo mbalimbali nchini ni kutowekwa wazi kwa haraka machapisho na Tafiti mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutang... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More