WAZIRI WA MADINI ANGELA KAIRUKI AWAPA ONYO WATOROSHAJI WA MADINI YA RUBY MUNDARARA LONGIDO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI WA MADINI ANGELA KAIRUKI AWAPA ONYO WATOROSHAJI WA MADINI YA RUBY MUNDARARA LONGIDO

WAZIRI wa Madini Angela Kairuki amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya Vito ya Ruby katika Kata ya Mundarara wilayani Longido mkoani Arusha kujitafakari upya na kuwa wakweli katika biashara hiyo ya madini.

Akiwa katika ziara yake ya kikazi iliyolenga kujionea shughuli za uchimbaji wa madini hayo ya vito pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili Waziri Kairuki alifanya pia mkutano mkubwa wa hadhara kijijini hapo. Akizungumza na wananchi hao wa Mundarara Waziri Kairuki aliwataka wananchi hao kushirikiana na Serikali katika kuwafichua watu wasiowaaminifu kwa rasilimali za taifa.

“Nyinyi wananchi na wafanyabiashara hapa mnawajua wanaotorosha madini kwenda nchi jirani, niwaombe muwafichue kwani madini hayo ni fedha mnazozihamishia nchi nyingine ambazo zingewaletea maendeleo nyinyi. “Tafadhaili sana kwa wafanyabiashara naowamba muache kuanzia sasa kwani mtajikuta mkiwa katika wakati mgumu wa kupteza mitaji yenu na hata kupoata hasara kubwa pindi mtakapok... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More