WAZIRI WA MAMBO YA NJE AZUNGUMZA NA MKURUGENZI WA AFRIKA KUTOKA NORWAY - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI WA MAMBO YA NJE AZUNGUMZA NA MKURUGENZI WA AFRIKA KUTOKA NORWAY

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Kusini mwa Afrika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Norway, Bw. Germund Saether. Katika mazungumzo hayo, walijadili umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Norway hususan katika sekta za kukuza uchumi kwa maendeleo ya mataifa haya mawili. Mazungumzo hayo yamefanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam tarehe 10 Mei 2019  Kulia ni Balozi wa Norway hapa nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen pamoja na maafisa kutoka ubalozi huo wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na mgeni wake (hawapo pichani).  Mazunguzmzo kati ya Mhe. Prof. Kabudi na Bw. Saether yakiendelea huku wajumbe wengine wakifuatilia. Pembeni kwa Mhe. Prof. Kabudi ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More