WAZIRI WA MICHEZO DK. MWAKYEMBE AZURU CHAMAZI NA KUSEMA AZAM FC NI KIWANDA CHA SOKA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI WA MICHEZO DK. MWAKYEMBE AZURU CHAMAZI NA KUSEMA AZAM FC NI KIWANDA CHA SOKA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, leo alifanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Azam FC ‘Azam Complex’ na kukiri kuwa timu hiyo ni kiwanda cha soka nchini.
Ziara hiyo ya Mwakyembe ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuangalia Azam FC ilipofikia kwenye uboreshaji wa uwanja huo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U-17) zitakazofanyika nchini mwakani.
Uwanja wa Azam Complex ni miongoni mwa viwanja vitatu nchini vilivyoteuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa kushirikiana na la hapa nchini (TFF), vingine viwili vikiwa ni Uwanja wa Taifa na ule wa Uhuru.

Waziri  wa Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa na viongozi wa Azam katika ziara yake ya Azam Complex leo

Kigogo huyo aliambatana na Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Alex Nkeyenge na Mkurugenzi wa Mashindano TFF, Salum Madadi, ambao walikaribishwa na wenyeji wao akiwemo... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More