Waziri wa Nishati afanya mazungumzo na washirika wa maendeleo - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waziri wa Nishati afanya mazungumzo na washirika wa maendeleo

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amekutana na washirika wa maendeleo wanaofadhili miradi ya nishati ili kujadiliana nao kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo miradi wanayoifadhili na miradi mipya inayohitaji fedha za uwekezaji.
Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma katika Ofisi za Wizara ya Nishati na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt Hamisi Mwinyimvua, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu,  Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi na watendaji kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara.
Baadhi ya washirika wa maendeleo waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Benki ya Dunia (WB), Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Ubalozi wa Ujerumani na Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania.
 “Serikali haiwezi kufanya kazi peke yake hasa katika kutekeleza mipango ya muda mrefu ya kuzalisha megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025 na mipango ya muda  mfupi ya kuzalisha megawati 5000 ifikapo mwaka 2020,” ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More