WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AZINDUA JENGO LA TAASISI YA UTAFITI WA AFYA ZANZIBAR - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AZINDUA JENGO LA TAASISI YA UTAFITI WA AFYA ZANZIBAR

Na Khadija Khamis –Maelezo ZanzibarWaziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Hussein Ali Hassan amesema tafiti za kisayansi za Afya zinasaidia kujua chanzo cha maradhi na tiba yake ikiwemo matumizi ya dawa asilia. Dk.Husein alieleza hayo Binguni Wilaya ya Kati Unguja wakati wa Ufunguzi wa Jengo la Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema tafiti za kisayansi ya afya katika nchi zinamchango mkubwa katika kupunguza maradhi kwani baadhi ya maradhi yanaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kutumia vyakula vya kawaida bila kutumia dawa za Hospitali. Aliwataka wananchi kupokea matokeo ya tafiti zitakazofanywa na Taasisi hiyo na Taasisi nyengine ili kuleta mabadiliko katika maisha yao.
Dkt. Hussein aliwashauri wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar kufanyakazi kwa juhudi na maarifa na  kuhakikisha mimea na dawa za asili zinazotumika kwa ziko katika hali ya usalama kwa matumizi ya binaadamu. Ali... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More