Wekezeni kwenye afya kwa kujiunga na NHIF- Waziri Ummy - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wekezeni kwenye afya kwa kujiunga na NHIF- Waziri Ummy

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Bernard Konga katika mkutano wa hadhara Halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba Mkoani Mtwara wakati wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na NHIF, kupitia Mpango wa Ushirika Afya.
Na Grace Michael
Wananchi Mkoani Mtwara wametakiwa kufanya uwekezaji kwenye afya zao kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili wawe na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote. Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na wananchi katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba mkoani Mtwara.
Amesema kuwa ili kila mwananchi aweze kuwa na uhakika wa kufanya shughuli zingine za maendeleo na uwekezaji mwingine lazima awe na uhakika na afya yake kwa kuwa na uhakika wa kupata matibabu.Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akikagua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More