WEMA SEPETU ATUPWA GEREZANI SEGEREA SIKU NANE - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WEMA SEPETU ATUPWA GEREZANI SEGEREA SIKU NANE

Msanii wa Filamu Wema Sepetu akitoka katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo baada ya mahakama hiyo kutoa maamuzi ya kwenda Gereza la Segerea kwa siku nane. Wema aliingia matatani baada ya kutofika mahakamani hapo mara mbili hivyo mahakama ilitoa hati ya kumkamata kwa kuruka dhamana.Msanii wa Filamu Wema Sepetu akiingia katika gari la magereza. Wema Sepetu akipaelekea kupanda gari la magereza baada ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa maamuzi ya kwenda Gereza la Segerea kwa siku nane. 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru msanii wa filamu Wema Sepetu kukaa  gerezani kwa siku nane wakati akisubiri maamuzi ya dhamana.
Wema aliingia matatani baada ya kutofika mahakamani hapo mara mbili hivyo mahakama ilitoa hati ya kumkamata kwa kuruka dhamana.
Akitoa maamuzi hayo leo, Hakimu Mkazi, Maira Kasonde alisema kutokana na  masuala yaliyoletwa mahakamani hapo yanahusu dhamana, atatoa uamuzi.
Alisema kesi hiyo itakuja Juni 24, mwaka huu hivyo mshitakiwa anatakiwa... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More