WEZI WA MAJI YA DAWASCO WAKAMATWA TEMBONI JIJINI DAR ES SALAAM - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WEZI WA MAJI YA DAWASCO WAKAMATWA TEMBONI JIJINI DAR ES SALAAM

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) leo limeendesha operesheni ya kuwakamata wale wote waliojiunganishia maji na mkufanya biashara ya maji bila ya kuwa na kibali. Akizungumza Kaimu Meneja wa DAWASCO mkoa wa Kimara, Frank Sulley amesema wameamua kuendelea na operesheni yao maana watu hao wamekuwa wakihujumu shirika hilo kwa kuiba maji huku wakiharibu miundo mbinu. 
"Leo tupo eneo la Kimara Temboni na tumewamata mama (jina kapuni) ambaye alikuw akifanya biashara ya maji na kuharibu miundo mbinu, kwa kukata bomba na kujaza tanki lake na kufanya biashara ya kuuza maji ambapo amekuwa akiuza tsh 6,000 kwa tanki la lita 1,000,' amesema Sulley. 
Amesema kuwa kumekuwa na mchezo wa kujiunganishia maji kwa njia ya kinyemela kwa kukata bomba nyuma ya mita na kutumia huku mita ikiwa haisomi jambo linalohujumu uchumi wa shirika hilo. Aliongeza kuwa amewataka wateja kujitokeza kujisalimisha wale wote waliojiunganishia kinyemela kabla ya muda hauja... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More