WHO yasema hakuna haja ya kutangaza hali ya hatari juu ya Ebola - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WHO yasema hakuna haja ya kutangaza hali ya hatari juu ya Ebola

Shirika la Afya duniani WHO, limetahadharisha juu ya hatari ya kuenea kwa maradhi ya Ebola yaliyolipuka nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


Mkurugenzi wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema hatari hiyo ipo kweli lakini Kamati ya dharura ya Shirika hilo, imesema hakuna haja ya kutangaza hali ya dharura kwa sababu ugonjwa huo haujasambaa kimataifa.


Hata hivyo watu wawili wamefariki katika nchi jirani ya Uganda, kutokana na maradhi hayo baada ya watu hao kuingia nchini humo kutokea Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


Katikati ya mwaka uliopita watu zaidi ya 2100, waliambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Congo na 1400 kati ya hao walifariki.Tweet


Source: Kwanza TVRead More