WIZARA YA AFYA YATAMBUA UMUHIMU WA MAMALAKA MAABARA YA SERIKALI YA MKEMIA MKUU KATIKA KULINDA AFYA ZA WANANCHI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WIZARA YA AFYA YATAMBUA UMUHIMU WA MAMALAKA MAABARA YA SERIKALI YA MKEMIA MKUU KATIKA KULINDA AFYA ZA WANANCHI

Na Chalila Kibuda, Globu ya JamiiMGANGA  Mkuu wa  Serikali  Profesa  Mohamed Kambi amesema Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inatambua umuhimu wa Mamlaka ya Maabara ya  Serikali Mkemia Mkuu katika kulinda ya afya ya wananchi.
Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto ambapo amesema kikao cha baraza  ni kuhakikisha kuna kuwepo kwa uhusiano kati ya watendaji na Menejimenti.Kambi amesema katika mkutano wa baraza wanatakiwa kujadili malengo ya taasisi na maslahi ya wafanyakazi ikiwemo mafunzo  ambayo yanatakiwa kutolewa kwa haki sawa.Aidha Mganga Mkuu huyo ametaka wafanyakazi  wa (GCLA) kuachana na kuwa sehemu ya watu wanaolalamika badala yake wanatakiwa kutatua changamoto zinazowakabili.Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi (GCLA), Dk. Fidelice  Mafumiko  amesema katika kikao  hicho watajadili ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More