WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAAHIDI KUENDELEZA TAFITI ZA TIBA ASILIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAAHIDI KUENDELEZA TAFITI ZA TIBA ASILIA

Na Ramadhani Ali – Maelezo                          Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazimmoja Dk. Ali Salum Ali amesema Wizara ya Afya itaendelea kufanya utafiti aina mbali mbali za mimea iliyopo Zanzibar ili kuzalisha dawa mpya za Tiba Asilia kwa ajilia ya kutibu maradhi mbali mbali.
Akizungumza katika mkutano wa Tafiti wa Tiba asilia ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) na kuwashirikisha wadau wa tiba hiyo na ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Tianjin cha China, Dk. Ali alisema dawa nyingi zinazotumika Hospitali zinatokana na mimea baada ya kufanyika tafiti mbali mbali za kisayansi.
Alisema kutokana na kutambua umuhimu wa mimea kwa ajili ya Tiba asilia, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na watibabu wa tiba hiyo ambao wanatumia mizizi, majani na magome ya mimea.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazimmoja aliweka wazi kuwa Zanzibar imepiga hatua katika matibabu ya Tiba asilia na sehemu nyingi watibabu wa t... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More