Wizara ya Mambo ya Nje yahamasisha uwekezaji katika sekta ya Kilimo na Mifugo - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wizara ya Mambo ya Nje yahamasisha uwekezaji katika sekta ya Kilimo na Mifugo

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda amefanya mazungumzo na kampuni ya Burmeister & Partiners (PTY) LTD ya nchini Namibia tarehe 10 Agosti 2018 mjini Windhoek, Namibia.
Akiongea na uongozi wa kampuni hiyo Prof. Mkenda alieleza Tanzania ina eneo kubwa la ardhi yenye rutuba ambayo haitumiki na rasilimali watu ya kutosha hivyo ni fursa kwa mwekezaji mwenye nia thabiti kuwekeza nchini.
“Lengo la Serikali ni kupata mwekezaji aliye makini kama wewe nimeona una mradi mkubwa wa shamba la mifugo na vifaa vya kisasa kwa ajili ya machinjio nina imani ukija kuwekeza Tanzania hautajutia kabisa kwakuwa matumizi ya teknolojia ya kisasa katika miradi itaongeza thamani ya mazao na bidhaa zitakazozalishwa na kuwezesha kupatikana kwa soko la kimataifa” alisema Prof. Mkenda
Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mhandisi Hendrik Boshoff alieleza kampuni imekuwa ikifanya kazi katika mataifa mbalimbali ambapo kampuni hiyo imefungua kampuni ya maziwa nchini R... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More