WIZARA YAWAKUMBUSHA WADAU KUHUSU UMUHIMU WA KULINDA MFUMO WA FEDHA NCHINI, KUDHIBITI UTAKATISHAJI FEDHA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WIZARA YAWAKUMBUSHA WADAU KUHUSU UMUHIMU WA KULINDA MFUMO WA FEDHA NCHINI, KUDHIBITI UTAKATISHAJI FEDHA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
WIZARA ya Fedha na Mipango kupitia Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) imeandaa warsha kuhusu udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi kwa wadau wa sekta ya fedha nchini.
Lengo la warsha hiyo ni kuendelea kuwakumbusha wadau kuhusu umuhimu wa kulinda mfumo wa fedha wa nchi yetu ili usitumiwe vibaya na wahalifu na watu wasio waaminifu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo kuhusu udhibiti wa utakatishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi, Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Onesmo Makombe alisema tatizo la utakasishaji wa fedha haramu ni tatizo kubwa ulimwenguni kote na katika jamii.
Amesema ni kwasababu ya kuwepo kwa vitendo mbalimbali vya uhalifu vinavyowapatia wahalifu pato haramu. Uhalifu huo ni pamoja na ukwepaji kodi, biashara haramu ya dawa za kulevya, biashara haramu ya watu, biashara haramu ya silaha, rushwa, kughushi, ujangili, uharamia, uvunaji haramu wa magogo, uuzaji wa bidh... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More