Wolper Amkingia Kifua Steve Nyerere Kwenye Suala la Rambirambi - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wolper Amkingia Kifua Steve Nyerere Kwenye Suala la Rambirambi

Msanii wa filamu za Bongo Movie Jacqueline Wolper ameibuka na kumkingia kifua msanii mwenzake Steve Nyerere na kumtaka asivunjike moyo kusaidia wengine.


Steve Nyerere amekuwa Kwenye headlines za mitandao ya kijamii kwa muda sasa huku skendo ambayo imekuwa ikimuandama ni ya kila pesa za rambi rambi anazokusanya Kwenye misiba ya watu.


Na ishu hii imerudi  kwa kasi Tena mara baada ya Steve Nyerere kuonekana akiwa mstari wa mbele siku ya leo kwa ajili ya kuandaa msiba wa msanii Mzee Majuto.


Wolper ameibuka na kumkingia Steve na kumpa moyo kwa kazi nzuri anayofanya ya kuwasaidia watu ambao ni wafiwa na kumtaka ayapuuze maneno ambayo yamekuwa yakisemwa juu yake:Kaka yangu Steve wewe ni miongoni wa watu wachache wenye moyo wapekee na wa kujitoa, Nimekua nikiona maneno kejeli na dharau mitandaoni zikiendelea juu yako ila nikiwa Kati ya watu wanaothamini mchango wako wa kujitoa kwa moyo haswahaswa kwenye matatizo ( misiba ) na hata raha nakuomba usivunjike moyo ,usikate tamaa kwa maana naamini hiyo ni karma uliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu. Najua unapitia kipindi kigumu kakaangu ila piga moyo konde na kuendelea kuifanya kazi yako kwa ufanisi ule ule kwa maana naamini ipo siku Mungu atakulipa. Binadamu tumeumbwa kuzungumza liwe jema liwe baya ila kwa unalolifanya ni wachache saana wenye moyo huo na jua kwamba tuko nyuma yako na tunakusupport. @stevenyerere2 Na hili la mzee wetu majuto tunakutegemea, Binafsi nakuamini na Niko nyuma yako. #Nakupenda..


A post shared by @ wolperstylish on Aug 8, 2018 at 4:37pm PDT

The post Wolper Amkingia Kifua Steve Nyerere Kwenye Suala la Rambirambi appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source: Ghafla TZRead More