Wolper amlilia Soudy Brown na Maua Sama, ajitosa kuwaombea msamaha ‘jamani ndani sio kuzuri’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wolper amlilia Soudy Brown na Maua Sama, ajitosa kuwaombea msamaha ‘jamani ndani sio kuzuri’

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Jacquiline Wolper amejikuta akiumia kwa tukio la kukamatwa kwa mtangazaji wa kipindi cha SHILAWADU Soudy Brown na Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Soudy Brown.


Related imageWolper

Wolper kupitia ukurasa wake wa Instagram, amesema anaomba viongozi wakubwa wa nchi wawaachie wasanii hao kwani walikuwa kwenye utafutaji na badala yake adhabu waliyoipata kwa siku hizi tatu liwe funzo kwa wengine.


Katika utafutaji Kuna mitihani Mingi Sana. Nachoweza kusema Nikuomba Tuu wakubwa muwasamehe vijana wenzetu Naamini katika Hili lililotokea Basi wengine wengi watajifunza kitu kupitia hili Naomba niwaombee masamaha wa Dhati kabisa Ndugu zetu Na wawe huru kuendelea Na majukumu yao inshallah. Maua & Soudy na wengine wore mliopo Ndani Juu ya hili sio sawa kutaja wote lakini hawa niwawakilishi poleni saanaa Jamani Ndani sio kuzuri,“ameandika Wolper.


Maua Sama na Soudy Brown wanatuhumiwa kwa kosa la uharibifu wa mali za umma kwani walichapisha video katika mitandao ya kijamii ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More