Wolper Awaombea Msamaha Soudy Brown na Maua Sama Wanaosota Rumande - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wolper Awaombea Msamaha Soudy Brown na Maua Sama Wanaosota Rumande

Msanii wa filamu za Bongo Movie na mjasiriamali Mrembo Jacqueline Wolper ameibuka na kuwaombea msamaha mtangazaji wa Clouds Fm Soudy Brown na msanii wa Bongo fleva Maua Sama.


Maua na Soudy wamewekwa ndani tangu siku ya Jumapili mpaka leo hawajapata dhamana baada ya kuonekana kwenye video clips wakiwa wanakanyaga pesa.


Wolper amejikuta akiguswa na kitendo hicho cha kuwekwa ndani ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram, amesema anaomba viongozi wakubwa wa nchi wawaachie wasanii hao kwani walikuwa kwenye utafutaji na badala yake adhabu waliyoipata kwa siku hizi tatu liwe funzo kwa wengine. Katika utafutaji Kuna mitihani Mingi Sana. Nachoweza kusema Nikuomba Tuu wakubwa muwasamehe vijana wenzetu Naamini katika Hili lililotokea Basi wengine wengi watajifunza kitu kupitia hili Naomba niwaombee masamaha wa Dhati kabisa Ndugu zetu Na wawe huru kuendelea Na majukumu yao inshallah. Maua & Soudy na wengine wore mliopo Ndani Juu ya hili sio sawa kutaja wote lakini hawa niwawakilishi poleni... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More