Yaelezwa maafisa Kenya wafukua mwili ili kuuvua sare za kazi, Fahamu zaidi - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Yaelezwa maafisa Kenya wafukua mwili ili kuuvua sare za kazi, Fahamu zaidi

Maafisa wa magharibi mwa Kenya wamefukua mwili wa mkaazi mmoja ili kumvua sare alizozikwa nazo kulingana na ripoti. Martin Shikuku Alukoye alizikwa akiwa na sare zake za huduma ya vijana wa kaunti ya kakamega baada ya kufa maji mwezi huu. Baadaye maafisa wa kaunti hiyo waliufukua mwili wake ili kumvua nguo hizo kulingana na ripoti.Mjombaake bwana Alukoye alisema kwamba walikiuka sheria za nchi na tamaduni. ”Tuliishirikisha kamili serikali ya kaunti katika mipango ya mazishi na hawakupinga pendekezo letu kumzika akiwa na sare za kazini”, alisema Francis Mutamba.


Familia hiyo inasema kwamba ilipinga ombi kutoka kwa maafisa kuchukua nguo hizo kufuatia kuzikwa kwa jamaa huyo mwenye umri wa miaka 31, na kwamba mafisa waliamua kuufukua mwili huo bila idhini yao au agizo la mahakama. Naibu huyo wa chifu wa eneo la Ituti , Daniel Namayi alishutumu ufukuzi huo na kuonya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya maafisa hao.


”Mara tu mwili unapozikwa , utahitaji agizo la mahakama kwa mtu yeyot... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More