Yaelezwa ndege zisizotumia rubani kukagua uchafu Dar Es Salaam, fahamu zaidi - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Yaelezwa ndege zisizotumia rubani kukagua uchafu Dar Es Salaam, fahamu zaidi

Kampuni ya Open Map Development Tanzania (OMDT) imezindua ndege zisizotumia rubani (drones) zitakazokuwa zinaangalia maeneo yaliyojificha yenye mkusanyiko wa uchafu unaozuia maji kutembea katika mitaro na kusababisha mafuriko na magonjwa ya milipuko wakati wa masika.Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jana Dar es Salaam, msimamizi wa teknolojia hiyo, Fredrick Mbuya alisema ndege hiyo itakuwa inatumiwa na watu wanaofanya shughuli za kukusanya taka katika maeneo mbalimbali na kwamba imewekewa mfumo ambao unaweza kugundua eneo lenye uchafu hata kama limejificha.


“Tunajua tuna changamoto   kubwa ya kutambua uchafu uliopo katika  maeneo mbalimbali, hasa katika mito na sehemu zenye miti mingi, hizi taka zinapojaa katika maeneo hayo zinazuia maji kutembea katika mifereji na kusababisha mafuriko katika kipindi cha mvua,” alisema Mbuya.


Alisema mbali na kuonyesha takataka zilipo, teknolojia hiyo pia itakuwa inaonyesha eneo la kwenda kutupa takataka hizo na  umbali wake kutoka ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More