YAHYA ZAYED ACHUKULIWA NA ISMAILIA YA MISRI KWA MKATABA WA MIAKA MITATU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YAHYA ZAYED ACHUKULIWA NA ISMAILIA YA MISRI KWA MKATABA WA MIAKA MITATU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Yahya Zayed anayechezea klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam ameomdoka jana mjini Dar es Salaam kwenda Misiri kujiunga na klabu ya Ismailia ya huko.
Zayed mwenye umri wa miaka 20 aliondoka kwa ndege ya shirika la Ethiopia moja kwa moja kwenda Cairo ambako imeelezwa akifika atasaini mkataba wa miaka mitatu.
Na hiyo ni baada ya Ismailia, moja ya klabu kongwe nchini Misri kumalizana na Azam FC juu ya mchezaji ambaye alikuwa amebakiza mkataba wa miaka miwili.  
Akisaini mkataba huo, Zayed atakuwa mchezaji wa pili wa Tanzania katika Ligi Kuu ya Misri, baada ya kiungo Himid Mao anayechezea Petrojet ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Azam FC.

Yahya Zayed (katikati) amekwenda Misiri kujiunga na klabu ya Ismailia kwa mkataba wa miaka mitatu

Himid, Nahodha Msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars yupo katika msimu wake wa kwanza Misri baada ya kujiunga na Petrojet Juni mwaka jana akitokea Azam FC aliyoanza kuic... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More