YANGA KUANZA NA WABOTSWANA, SIMBA MSUMBIJI MICHUANO YA CAF - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA KUANZA NA WABOTSWANA, SIMBA MSUMBIJI MICHUANO YA CAF

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Shirikisho la Mpira Afrika CAF wametoa ratiba ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika (CCL) ambapo wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano hiyo Simba na Yanga zikipangiwa timu kutoka ukanda wa Jangwa la Sahara.
Mabingwa wa Tanzania Simba wataanzia ugenini dhidi ya timu ya UD do Songo ya Msumbiji kati ya tarehe 09/10/11 Agosti 2019 nchini Msumbiji.
Mshindi wa mchezo kati ya Simba na UD do Songo atacheza na mshindi kati ya Nyasa Big Bullets ya Malawi na Platnumz ya Zimbabwe.
Wawakilishi wengine wa michuano hiyo Yanga wataanzia nyumbani dhidi ua Township Rollers mchezo utakaochezwa kati ya tarehe 09/10/11 Agosti 2019 na baadae kurudiana nao nchini Botswana.
Mshindi wa mchezo huo atamsubiri mshindi kati ya Green Mamba Eswatin na Zesco ya Zambia.Kwa upande wa wawakilishi kutoka Zanzibar, KMKM watarusha karata yao ya kwanza kwa Desportivo De 1 Agosto ya Angola na mshindi wa mchezo huo atamsubiri na Green Eagles ya Zambia dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Kw... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More