YANGA KUWAFUATA MWADUI JUMANNE LIGI KUU BARA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA KUWAFUATA MWADUI JUMANNE LIGI KUU BARA


MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc, kwenye uwanja wa Majaliwa, Lindi, siku ya Jumapili, Kikosi cha Yanga, kitarejea Dar es Salaam siku ya Jumatatu, tayari kwa kukwea ‘pipa’ Jumanne alfajiri kueleka Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya wenyeji Mwadui Fc uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Kambarage.

 Ofisa habari wa kikosi hicho Dismas Ten ameweka wazi kuwa matayarisho yote kwa ajili ya safari hiyo yanakwenda vizuri, na kinachosubiriwa sasa ni wakati tu kuweza kufanya safari hiyo.
"Kama ambavyo unafahamu, jumapili timu yetu itakuwa Lindi kwenye uwanja wa Majaliwa, kucheza mchezo wa kirafiki na Namungo Fc, baada ya mchezo huo tunatarajia kikosi kitarejea Dar siku ya jumatatu asubuhi na jumanne alfajiri itasafiri kwenda Shinyanga, kwa ajili ya mchezo wa ligi siku ya alhamisi.,"amesema Ten.


Akiendelea zaidi Ten alisema kuwa, wanafahamu ubora wa Mwadui Fc ikiwa inacheza uwanja wa Kambarage, hivyo Yanga ina kila sababu ya kujiandaa vyema ili kuweza kupat... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More