YANGA SC INAHITAJI KOCHA WAKE WA KUWA KAZINI MUDA WOTE SI ZAHERA ANAYETUMIKIA ‘MABWANA WAWILI’ - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA SC INAHITAJI KOCHA WAKE WA KUWA KAZINI MUDA WOTE SI ZAHERA ANAYETUMIKIA ‘MABWANA WAWILI’

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
WAKATI Mbelgiji, Patrick Aussems aliiongoza Simba SC kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya African Lyon jana, Yanga SC itamkosa kocha wake Mkuu, Mwinyi Zahera ikimenyana na Mbao FC kuanzia Saa 1:00 usiku wa leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. 
Zahera pamoja na kuwa kocha Mkuu wa Yanga SC, bado anaendelea kuwa Kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), maarufu The Leopard, yaani Chui – wakati Aussems ni kocha wa Simba tu, analala anaota na anashinda anawaza na kutumikia bwana mmoja tu.
Na wakati huu wa mapumziko ya kupisha mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Cameroon, Zahera amekwenda kuungana na mkuu wake, Florent Ibenge kuiandaa timu yao kwa ajili ya mchezo wa Kundi G dhidi ya Zimbabwe Jumamosi ijayo mjini Kinshasa.

Mwinyi Zahera (katikati) akiwa na Kocha Msaidizi, Mzambia, Noel Mwandila (kulia) na Mratibu, Hafidh Saleh (kushoto)

Za... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More