Yanga SC kuelekea Iringa leo kuwafuata Lipuli FC - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Yanga SC kuelekea Iringa leo kuwafuata Lipuli FC


Kikosi cha Yanga SC kinatarajia kuanza safari ya kuelekea mkoani Iringa kwaajili ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara utakaochezwa Machi 16 mwaka huu katika Uwanja wa Samora.

Mratibu wa Klabu hiyo Hafidhi Salehe amesema kuwa baada ya mazoezi ya leo kumalizika katika Viwanja vya polisi, Kikosi cha wachezaji 20 pamoja na benchi la ufundi watasafiri kesho kuelekea Iringa kuivaa Lipuli FC.
.
"Tumemaliza salama mazoezi hapa katika Uwanja wa Polisi kurasini na kesho asubuhi tutaanza safari ya kuelekea mkoani Iringa kwa ajili ya mchezo wetu wa jumamosi dhidi ya Lipuli,Lipuli ni timu nzuri lakini tangu wapande Ligi kuu tumekuwa tukipata matokeo mazuri kila tukionana nao na tunaimani katika mchezo wetu wa jumamosi tutafanya vizuri pia" amesema Salehe

Yanga anakutana na Lipuli akiwa anashika nafasi ya kwanza na point 67 kwenye msimamo wa Ligi huku Lipuli FC ikishika nafasi ya Sita akiwa na point 41.... Continue reading ->Source: Mwanaharakati MzalendoRead More