YANGA SC KUENDELEA KUMKOSA MAHADHI LAKINI ‘NINJA’, ABDUL, YONDAN NA KAMUSOKO WAMEREJEA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA SC KUENDELEA KUMKOSA MAHADHI LAKINI ‘NINJA’, ABDUL, YONDAN NA KAMUSOKO WAMEREJEA

Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga SC itaendelea kumkosa kiungo wake, Juma Mahadhi baada ya kuumia katika mchezo Agosti 19 mwaka huu kwenye mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger ya Algeria. 
Mahadhi aliingia kipindi cha pili kwenda kuchukua nafasi ya kiungo Pius Buswita, lakini hakumaliza mchezo baada ya kuumia naye akampisha Ibrahim Ajib.
Maumivu hayo yameendelea kumuweka nje na leo Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kwamba mchezaji huyo amepewa mapumziko ya kujiugiza zaidi. 
Hafidh amesema kwamba majeruhi wengine waliokosekana kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya African Lyon Jumapili Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Yanga ikishinda 1-0, mabeki Juma Abdul, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Kelvin Yondani na kiungo Thabani Kamusoko wamepona. 
Juma Mahadhi (kushoto) ataendelea kukosekana Yanga SC baada ya kuumia Agosti 19, mwaka huu

Hafidh amesema kwamba watatu hao wamejiunga na wachezaji wenzao mazoezini, Uwanja wa Chuo cha Maofisa wa Jeshi la Polisi, ... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More