YANGA SC KUMENYANA NA AFC LEOPARDS JUMAPILI MECHI YA KIRAFIKI SHEIKH AMRI ABEID - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA SC KUMENYANA NA AFC LEOPARDS JUMAPILI MECHI YA KIRAFIKI SHEIKH AMRI ABEID

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Yanga SC itamenyana na AFC Leopards ya Kenya Jumapili Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha katika mchezo wa kirafiki.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Frederick Mwakalebela amesema leo katika mkutano na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Jangwani mjini Dar es Salaam kwamba maandalizi ya mchezo huo yamekamilika. 
Utakuwa mchezo maalum wa mwisho wa kujiandaa na mechi ya marudiano Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Township Rollers utakaofanyika Agosti 24 Uwanja wa Taifa mjini Gaborone.
Na utachezwa siku mbili baada ya mchezo mwingine wa kwanza wa kirafiki, dhidi ya Polisi Tanzania Ijumaa mjini Moshi, pia kujiandaa na mechi dhidi ya Township Rollers.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Frederick Mwakalebela (kulia) akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari leo 

Yanga inayofundishwa Kocha Mkongo, Mwinyi Zahera imewasili mjini Moshi mkoani Kilimanjaro leo kuweka kambi wa kujiandaa na mchezo dhidi ya Township Rollers.
Ha... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More