YANGA SC KUMENYANA NA AS VITA AGOSTI 4 TAIFA KATIKA KILELE CHA SIKU YA MWANANCHI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA SC KUMENYANA NA AS VITA AGOSTI 4 TAIFA KATIKA KILELE CHA SIKU YA MWANANCHI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga itamenyana na vigogo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), AS Vita katika mchezo wa kirafiki Agosti 4, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Mchezo huo utafanyika katika kilele cha Wiki Mwanachi, tamasha maalum la kutambulisha kikosi kipya cha klabu pamoja na jezi za msimu.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Frederick Mwakalebela amesema kwamba Wiki Mwanachi itaanza Julai 28 na kufikia kilele Agosti 4 na kuwakuw ana mchezo wa kirafiki dhidi ya AS Vita.
“Mbali na masuala ya kijamii ambayo yametengenezewa utaratibu na ratiba itakayosambazwa katika matawi yote ya klabu nchi nzima na groups zote za whatsap za Yanga, kadhalika na vyomba vya habari,”.

Mwakalebela amesema kwamba baada ya uzinduzi rasmi itafuata shoo kabambe ya mtaa kwa mtaa lengo ni kukusanya idadi kubwa ya wananchi.
“Wana Yanga wajiandae kwa burudani kutoka wa wasanii, waimbaji, waigizaji, pamoja na zawadi kemkem katika kusanya kusanya kusanya hii, hakika haijwahi tokea kati... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More