YANGA SC WAENDA KAMBINI MOSHI KUJIANDAA KWA MARUDIANO NA TOWNSHIP ROLLERS - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA SC WAENDA KAMBINI MOSHI KUJIANDAA KWA MARUDIANO NA TOWNSHIP ROLLERS

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha Yanga SC kitaondoka kesho Dar es Salaam kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Township Rollers Agosti 24 Uwanja wa Taifa mjini Gaborone.
Kocha Mkongo, Mwinyi Zahera alihitaji kambi katika mji wenye hali ya hewa ya baridi sawa na Gaborone na uongozi umeamua kuipeleka timu Moshi ambako ikiwa huko itacheza pia mechi mbili za kujipima nguvu.
Yanga SC inahitaji ushindi wa ugenini lazima ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo, kufuatia kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 nyumbani, Jumamosi na Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Siku hiyo, Yanga SC ilitanguliwa kwa bao la dakika ya saba tu lililofungwa na Phenyo Serameng, kabla ya kiungo Mnyarwanda, Patrick Sibomana kuisawazishia ‘Timu ya Wananchi’ dakika ya 86. 
Serameng alifunga bao lake baada ya kumpindua beki wa kushoto wa Yanga SC, Muharami Issa ‘Marcelo’ kufuatia pasi ya Kanogelo Matsa... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More