YANGA SC WAIFUATA MWADUI FC KWA NDEGE MECHI NI ALHAMISI UWANJA WA KAMBARAGE MJINI SHINYANGA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA SC WAIFUATA MWADUI FC KWA NDEGE MECHI NI ALHAMISI UWANJA WA KAMBARAGE MJINI SHINYANGA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha Yanga SC kimeondoka Alfajiri ya leo kwa ndege kwenda Mwanza kuunganisha usafiri wa barabara kwenda Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Alhamisi Saa 10:00 jioni Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Yanga SC inaondoka siku moja tu baada ya kurejea jana Dar es Salaam kutoka Lindi, ambako juzi ilicheza mechi ya kirafiki na kutoa sare ya 1-1 na wenyeji, Namungo FC Uwanja wa Majaliwa huko Ruangwa.
Wachezaji wote wa Yanga SC wakiwemo waliokuwa na timu za taifa wamesaifiri na ndege ya shirika la Tanzania (ATC) kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa wa 11 wa msimu kwao.
 
Kocha Mwinyi Zahera amerejea kutoka kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipokwenda kwa majukumu ya timu yake ya taifa lakini hajasafiri na timu na ataungana nao kesho amebaki Dar es Salaam kwa mapumziko. 
Kwa ujumla Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea kesho baada ya kusimama kupisha mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More