YANGA SC YAANZA NA SARE LIGI YA MABINGWA, YATOKA 1-1 NA TOWNSHIP ROLLERS TAIFA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA SC YAANZA NA SARE LIGI YA MABINGWA, YATOKA 1-1 NA TOWNSHIP ROLLERS TAIFA

Na Asha Said, DAR ES SALAAM
YANGA SC imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Yanga SC inayofundishwa na kocha Mwinyi Zahera raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) sasa inakabiliwa na zoezi la kwenda kuupanda mlima wiki ijayo mjini Gaborone kwa kulazimisha ushindi wa ugenini, au sare ya kuanzia 2-2 ili isonge mbele kwa faida ya mabao ya ugenini.  
Leo Yanga SC ilitanguliwa kwa bao la dakika ya saba tu lililofungwa na Phenyo Serameng, kabla ya kiungo Mnyarwanda, Patrick Sibomana kuisawazishia ‘Timu ya Wananchi’ dakika ya 86. 

Mshambuliaji wa Yanga SC, Mnamibia Sadney Urikhob (kulia) akimiliki mpira mbele ya beki wa Township Rollers leo Uwanja wa Taifa

Serameng alifunga bao hilo baada ya kumpindua beki wa kushoto wa Yanga SC, Muharami Issa ‘Marcelo’ kufuatia pasi ya Kanogelo Matsabu na kufumua shuti la kiufundi kwa mguu wake wa kus... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More