YANGA SC YACHEZA VYEMA NA KUICHAPA USM ALGER 2-1 MBELE YA MANJI…MAKAMBO MTU KWELI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA SC YACHEZA VYEMA NA KUICHAPA USM ALGER 2-1 MBELE YA MANJI…MAKAMBO MTU KWELI

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
YANGA SC imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuilaza mabao 2-1 USM Alger ya Algeria usiku huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Yanga SC inapanda nafasi ya tatu katika Kundi D ikifikisha pointi nne baada ya kufungwa mechi tatu awali na kutoa sare moja – kuelekea mchezo wa mwisho wa ugenini dhidi ya Rayon Sport nchini Rwanda wiki ijayo.
Katika mchezo wa leo, Yanga SC ilionyesha mabadiliko makubwa ya kichezaji baada ya muda mrefu wa kucheza ovyo na kuwaudhi mno mashabiki wake.
Ikiongozwa kwa mara ya kwanza na kocha wake mpya, Mkongo Mwinyi Zahera, Yanga SC ilipata bao lake la kwanza dakika ya 43 kupitia kwa kiungo Deus Kaseke aliyetumia makosa ya mabeki wa USM Alger na kumchambua kipa Mohammed Lamine.
Wafungaji wa mabao ya Yanga SC leo, Eritier Makambo (kulia) na Deus Kaseke (kushoto)
Mfungaji wa bao la kwanza la Yanga, Deus Kaseke akimtoka mchezaji wa USM Alger 
Mfungaji wa ... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More