YANGA SC YAFANYA MAUAJI MOROGORO, YAWATANDIKA TANZANITE 5-1 MECHI YA KIRAFIKI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA SC YAFANYA MAUAJI MOROGORO, YAWATANDIKA TANZANITE 5-1 MECHI YA KIRAFIKI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha Yanga SC leo asubuhi kimeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Tanzanite Centre ya Morogoro katika mchezo wa kirafiki mjini humo.
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Mkongo Herithier Makambo, Mrisho Ngasa, Deus Kaseke, Emmanuel Martin na Maka Edward.
Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya, lakini pamoja na mchezo ujao wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger Agosti 19, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na ile wa mwksho wa dhidi ya Rayon Sport Agosti 28 mjini Kigali, Rwanda.

Mrisho Ngassa (kushoto) akimhadaa mchezaji wa Tanzanites Centre leo Morogoro

Lakini kabla ya hapo, Jumapili wiki hii Yanga SC itakuwa na mchezo maalum wa kirafiki wa kumuaga aliyekuwa Nahodha wake, Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye baada ya kuichezea klabu hiyo tangu mwaka 2006, Cannavaro amestaafu mwishoni mwa msimu uliopita na kuwa Meneja wa timu.
Yanga SC haijashinda mechi hata moja ya Kombe la Shirikisho la Afrika katika kundi lake, baada ya ku... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More