YANGA SC YAREJEA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUIPIGA RUVU SHOOTING 1-0 LEO UHURU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA SC YAREJEA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUIPIGA RUVU SHOOTING 1-0 LEO UHURU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
YANGA SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 83 baada ya kucheza mechi 36, sasa ikiwazidi pointi moja, mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi tatu mkononi.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Hussein Athuman wa Katavi aliyesaidiwa na John Kanyenye wa Mbeya na Agness Pantaleo Arusha, bao pekee la Yanga SC lilifungwa na kiungo Papy Kabamba Tshishimbi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Tshishimbi alifunga bao hilo dakika ya 15 akimalizia pasi ya Deus David Kaseke alipokea pasi ya kichwa ya Raphael Daudi Lothi, wote viungo kufuatia majaro iliyoingizwa na beki wa kushoto, Mwinyi Hajji Mngwali.
Kipindi cha pili timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu, lakini Yanga SC ikafanikiwa kulinda bao lake na kubeba pointi tatu za mchezo huo.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Mwaduo FC i... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More