YANGA SC YATOZWA FAINI SH. MILIONI 3.5, YONDAN AFUNGIWA NA FAINI 500,000 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA SC YATOZWA FAINI SH. MILIONI 3.5, YONDAN AFUNGIWA NA FAINI 500,000

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga imetozwa faini ya Sh. Milioni 3 kwa kosa la kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC Aprili 4, mwaka huu Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. 
Taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, maarufu kama Kamati ya Saa 72 imesema kwamba hilo ni kosa la nne kwa Yanga SC msimu huu kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi, na adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14 (49) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Taratibu za Mchezo.
Aidha, Yanga pia imetozwa faini ya Sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kuwarushia chupa za maji waamuzi wakati wakirejea vyumbani baada ya mechi hiyo kumalizika.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Klabu.
Naye beki wake, Kelvin Yondani amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Sh. 500,000 baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More