YANGA YAICHAPA 1-0 MAWENZI MARKET 1-0, CANNAVARO AMKABIDHI NINJA ‘SILAHA ZAKE’ - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA YAICHAPA 1-0 MAWENZI MARKET 1-0, CANNAVARO AMKABIDHI NINJA ‘SILAHA ZAKE’

Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
BAO pekee la mshambuliaji mpya, Haritier Makambo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) limeipa ushindi wa 1-0 Yanga SC dhidi ya Mawenzi Market katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Huo unakuwa ushindi wa kwanza wa Yanga SC ndani ya mechi sita, tangu iliposhinda mara ya mwisho Jumanne ya Mei 22 bao 1-0 dhidi ya Mbao FC, bao pekee la kiungo Mzimbabwe, Thabani Scara Kamusoko aliyemtungua kwa shuti la mpira wa adhabu, kipa wa mkopo Metacha Boniphace Mnata kutoka Azam FC dakika ya 26.
Baada ya hapo, ilitoa sare mchezo uliofuata wa Ligi Kuu 2-2 na Ruvu Shooting FC Uwanja wa Taifa kabla ya kwenda kufungwa mechi nne mfululizo, 3-1 na Azam FC Ligi Kuu Taifa, 3-1 na Kakamega Homeboyz FC Nakuru nchini Kenya michuano ya SportPesa Super Cup, kabla ya kufungwa mara mbili mfululizo na Gor Mahia 4-0 mjini Nairobi na 3-2 Dar es Salaam Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika.
Mchezo wa leo ulikuwa maalum wa kumuaga aliyekuwa Nahodha wa klabu k... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More