YANGA YAPEWA BIASHARA UNITED, AZAM FC NA PAMBA 32 BORA KOMBE LA TFF - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA YAPEWA BIASHARA UNITED, AZAM FC NA PAMBA 32 BORA KOMBE LA TFF

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga SC itamenyana na Biashara United katika hatua ya 32 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kati ya Januari 25 na 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. 
Katika droo iliyopangwa leo makao makuu ya Azam TV, mshindi kati ya Yanga SC na Biashara United atamenyana na mshindi kati ya Mighty Elephant na Namungo FC katika hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo. 
Nao mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar watamenyana na Maji Maji FC ya Songea, wakati vigogo wengine, Azam FC watamenyana na Pamba SC ya Mwanza.
Kama ilivyo kwa Yanga, Azam FC nao watacheza nyumbani Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam na Mtibwa Sugar watacheza nyumbani Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Biashara United watarudi Dar es Salaam kumenyana tena na Yanga katika hatua ya 32 Bora kombe la TFF

Mechi nyingine za hatua ya 32 Bora ni kati ya Mashujaa FC ya Kigoma iliyowatoa Simba SC dhidi y... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More