YANGA YASHINDWA KUFURUKUTA DHIDI YA NDANDA UWANJA WA TAIFA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

YANGA YASHINDWA KUFURUKUTA DHIDI YA NDANDA UWANJA WA TAIFA

Na  Agness Francis, Globu ya Jamii. 
TIMU ya Yanga imetoshana nguvu na Ndanda FC 'wanakuchele' kwa kushindwa kupata alama 1 nyumbani kwa kutoka sare ya mabao 1-1 katika mchezo uliopigwa katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mtanange huo wa aina yake ulioanza majira ya saa moja usiku na kila upande wakicheza kwa kukamiana kutafuta magoli ya ushindi ambapo kwa kipindi cha kwanza dakika 15 za mapema tu Ndanda anapata goli la kuongoza kupitia kwa mchezaji wake Vitalis Mayanga alieingiza Mpira kimnyani na kutikisa nyavu za Yanga. 
Wachezaji walionekana kuinuka zaidi wakishambuliana kwa kila upande ukiitaji matokeo zaidi lakini mpira uligeuka kwa upande wa  Yanga kuwashambulia wapinzani wao na dakika ya 24 Jafari Mohamed anaindikia Yanga goli la kusawazisha kwa pasi iliyopigwa na Ibrahim Ajibu, Ambapo wachezaji wa Yanga walionekana kupata nguvu kwa kufanya mashambulizi katika lango la Ndanda ambayo hayakuleta matokeo,na mpaka wachezaji wanaenda mapumzikoni matokeo yalikuwa ni 1-1.Kipind... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More