'YES WE CAN' YAIPA SIMBA USHINDI WA 3-0 DHIDI YA JS SAOURA, DK.MWAKYEMBE ATOA NENO KWA MASHABIKI WA SOKA TANZANIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

'YES WE CAN' YAIPA SIMBA USHINDI WA 3-0 DHIDI YA JS SAOURA, DK.MWAKYEMBE ATOA NENO KWA MASHABIKI WA SOKA TANZANIA


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

YES We Can!Ndivyo unavyoweza kuuzungumzia ushindi wa timu ya Simba wa mabao 3- 0 dhidi ya timu ya JS Saoura katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Slaam.

Kabla ya mchezo huo uliofanyika jana jioni ya Januari 12,2019 ,Simba kupitia Msemaji wake Hajji Manara walizundua kampeni ya Yes we can ambayo kwa tafsiri ya Kiswahili inasema Ndio Tunaweza kwa lengo la kuhakikisha wanashinda mchezo huo na ndicho kilichotokea.

Umahiri,umaridadi wa pasi, akili ya soka na kila aina ya udambwidambwi kwa wachezaji wa Simba ulitosha kuwafanya wachezaji wa timu ya JS Saoura kushindwa kumiliki vema mpira na hivyo wachezaji wa Simba kuonekana kuumiliki kila idara.

Dakika ya 45 mshambuliaji nyota wa Simba Emmanuel Okwi alipeleka shangwe,nderemo na vifijo kwa Simba na mashabiki wa soka nchini baada ya kupachika bao la kwanza.Uwanja mzima ulizizima kwa shangwe kutoka kwa mashabiki na wapenzi wa Simba .Hivyo wakati wanakwenda mapumziko Simba walikuwa mb... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More