ZAHERA KIBOKO AKUTANA NA YONDANI, ATOA MPYA - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ZAHERA KIBOKO AKUTANA NA YONDANI, ATOA MPYA


Kocha huyo mwenye uraia wa DR Congo na Ufaransa, alisema kwamba wakati anaanza kukinoa kikosi hicho alionekana kugombana na Ajibu juu ya nidhamu lakini amejirekebisha kwa kiasi kikubwa na sasa ni mfano wa kuigwa.

Yondani awali alikuwa nahodha msaidizi lakini baada ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kustaafu akawa nahodha mkuu akisaidiwa na Juma Abdul ambaye ni swahiba wake mkubwa.

“Nimesikia watu wengi wakisema juu ya uamuzi wangu wa kumuondoa Yondani katika nafasi hii, naomba tu watu wote wajue kuwa sijakurupuka kufanya hivi kwani hata Yondani mwenyewe anajua kuwa kulikuwa na siku ningekuja kuchukua tu uamuzi kama huu kwani nilishamwambia abadilike lakini hakutaka kufuata maagizo yangu kwa wakati.


“Yondani amekuwa nahodha pamoja na Juma Abdul, lakini kwa nini sigombani na Juma nagombana na yeye tu, inabidi watu wafahamu kuwa siwezi kuwa na kiongozi ambaye yeye ndiye anaonekana chanzo cha kuwafanya wengine nao wakose nidhamu.

“Yondani amekuwa akifanya makosa kama haya ninamvumilia sana ... Continue reading ->

Source: Mwanaharakati MzalendoRead More