Zamaradi Mketema ageuka mbogo mtandaoni, aandika waraka mzito ‘siku hizi wachawi wamehamia Instagram’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Zamaradi Mketema ageuka mbogo mtandaoni, aandika waraka mzito ‘siku hizi wachawi wamehamia Instagram’

Mtangazaji wa TV na Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Zamaradi Mketema ameamua kuweka wazi kuhusu tuhuma zinazosambaa mtandaoni kuwa aliwachangisha watu fedha ili aweze kukamilisha zoezi la 40 ya mtoto wake King Salah.


Zamaradi akiwa kwenye sherehe za 40 ya mtoto wake King Salah

Zamaradi ameamua kuandika waraka mrefu kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akiweka baadhi ya risiti za malipo aliyoyafanya ili kuudhuhirishia umma kuwa hakulipisha wala kuchangisha watu kwenye sherehe hiyo ya 40 ya mtoto wake.


Kwa upande mwingine, Zamaradi amedai kuwa siku wachawi wamehamia kwenye mtandao wa Instagram kwani kumekuwa na watu wengi ambao hawapendi maendeleo ya wengine “Wachawi walikuwa wanajificha wanasubiri giza liingie wapae, ila siku hizi wachawi wamehamia Instagram wazi kabisa, wanapoona kuna mafanikio.


Imenilazimu niongee haya kwa minajili ya kulinda BRAND YANGU na watu NILIOINGIA NAO MKATABA KWASASA hivyo mniwie radhi nitaowakwaza.


Zamani wachawi walikuwa wanajificha wanasubiri giz... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More