Zari Aamua Kumuiga Wema Kwa Hili - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Zari Aamua Kumuiga Wema Kwa Hili

Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ amemuiga Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu kwa jina.


Ikiwa jina la Tanzania Sweetheart bado lina utata ambapo Wema Sepetu na  Hamisa Mobetto bado wako vitani kwa ajili ya Jina hilo na Zari naye ameibuka na lake.


Zari na yeye ameamua kumuiga kwa kujiita Uganda’s Sweetheart. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Snapchat, Zari aliweka picha yake na kuambatanisha na maneno hayo ya Uganda’s Sweetheart hali ambayo ilisababisha gumzo mitandaoni.


Mh! Bi dada naye kaona amuige Wema kwa kujipa jina la Sweetheart, makubwa,” alichangia mmoja wa wadau wa mtandao wa Instagram baada ya kipande hicho cha picha kusambaa.


Hata hivyo Zari hakutoa maelezo yoyote kama kujiita vile ilikuwa ni kwa ajili ya utani au kweli alimaanisha kutaka kuwa Uganda Sweetheart.


The post Zari Aamua Kumuiga Wema Kwa Hili appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More