Zari awajia juu mashabiki wanaomtaka ahame kwenye ya Diamond ya Afrika Kusini ‘sitoki, nilitumia akili kununuliwa’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Zari awajia juu mashabiki wanaomtaka ahame kwenye ya Diamond ya Afrika Kusini ‘sitoki, nilitumia akili kununuliwa’

Mwanamama Mjasiriamali, Zari ambaye pia ni mzazi mwenzie na Diamond Platnumz amejikiuta akishindwa kuvumilia maoni ya mashabiki wake mtandaoni wanaomtaka aondoke kwenye nyumba ya kifahari ya mzazi mwenzie, Chibu Dangote.


Zari na Diamond wakiwa kwenye nyumba hiyo Afrika Kusini

Zari kupitia ukurasa wake wa Intagram amesema kuwa hawezi kutoka kwenye nyumba hiyo, kwani yeye na watoto wake (Tiffah na Nillan) walinunuliwa nyumba hiyo ya kuishi.


Mrembo huyo kutoka Uganda Uganda ambaye makazi yake kwa sasa yapo Afrika Kusini, amesema kuwa kung’ang’ania kwake sio kwamba hana nyumba nyingine hapana anamiliki nyumba nne Afrika Kusini, bali anaishi kwenye nyumba hiyo kwani ni ya kwake na watoto wake.Diamond na Zari wameachana mapema mwaka huu baada ya kuishi kwa takribani miaka mitatu kwenye mahusiano, wamefanikiwa kupata watoto wawili Tiffah ambaye ndio mtoto wa kwanza wa Diamond na Nillan.


 


 


The post Zari awajia juu mashabiki wanaomtaka ahame kwenye ya Diamond ya Afrika Kusini ‘sitoki... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More