Zawadi za milioni 30 kushindaniwa Rock City Marathon - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Zawadi za milioni 30 kushindaniwa Rock City Marathon

Mwanza, 9 Oktoba 2018: Washindi wa michuano ya Rock City Marathon 2018 wanatarajiwa kuondoka na zawadi zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 30 pamoja na medali, imefahamika. Mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Akizungumza jijini Mwanza leo, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo zinazoratibiwa na kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Zenno Ngowi alisema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh.mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi kumi nao pia wakiibuka na medali na pesa taslimu.
Kwa upande wa mbio za Kilomita 21, Ngowi alisema, pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 3/- kila mmoja, sh. Mil 1/- kwa washindi wa pili na sh. 750,000/- kwa washindi wa tatu huku washindi wanne hadi wa kumi wakiibuka na zawadi za pesa taslimu na medali ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More