ZIARA TUMEJIFUNZA NA MAMBO MENGI SANA -MWAMUNYANGE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ZIARA TUMEJIFUNZA NA MAMBO MENGI SANA -MWAMUNYANGE

Na Zainab Nyamka, Globu ya JamiiBodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wamehitimisha ziara ya siku tatu ya kutembelea miradi mbalimbali inayosimamiwa na Mamlaka hiyo. Ziara hiyo iliyokuwa ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani imemalizika kwa Mwenyekiti wa bodi Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange kutoa tathmini ya jumla ya mambo waliyojifunza.
Akizungumza baada ya kuhitimisha ziara hiyo, Jenerali Mstaafu Mwamunyange amesema wananchi wana matarajio makubwa na DAWASA ya kupata huduma ya majisafi inayoaminika. Mwamunyange amesema kwenye ziara ya siku tatu wamejifunza mengi sana na wameona ni namna gani DAWASA wanafanya jitihada kubwa kuhakikisha wanafikisha maji kwa wananchi wote ili kufikia malengo ya serikali.
Amesema kuwa,  pamoja na yote kuna changamoto zinazoikabili DAWASA ikiwa ni pamoja na kupasuka kwa mabomba kutokana na miundo mbinu chakavu na kupelekea kupotea kwa maji mengi na watu wanaojiunganishia maji kiholela kitu kinachopelekea Mamlaka... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More