ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM PEMBA LEO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM PEMBA LEO

NA IS-HAKA, ZANZIBAR.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Dk.Bashiru Ally amesema CCM inaendelea kuimarika na hakuna Chama chochote cha kisiasa nchini kinachoweza kushindana nacho katika uringo wa siasa za ushindani wa sera za maendeleo kwa wananchi wa makundi yote.
Kauli hiyo aliitoa mara baada ya kuwasili kisiwani Pemba katika mwendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha ambapo amezungumza na wanachama mbalimbali katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Fidel Castro Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema kutokana na uimara huo hakuna chama kingine mbadala wa Chama Cha Mapinduzi kinachoweza kushuka kwa wananchi nyumba kwa nyumba na kuratibu kero zao kisha kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Dk.Bashiru aliwahakikishia wanachama na viuongozi hao kuwa CCM bado ipo imara na itapata ushindi wa kihistoria mwaka 2020 kwa nchini nzima kuliko ushindi unaopatikana kwa sasa katika uchaguzi mdogo unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini. KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More