“Zilipopigwa risasi hewani, Mbowe alikimbia mpaka miwani ikadondoka” Shahidi afunguka Mahakamani kesi ya viongozi wa CHADEMA - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

“Zilipopigwa risasi hewani, Mbowe alikimbia mpaka miwani ikadondoka” Shahidi afunguka Mahakamani kesi ya viongozi wa CHADEMA

Ushahidi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwamo Mwenyekiti Taifa, Freeman Mbowe, uliotolewa na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Gerard Rich, umedai kwamba aliamuru kikosi cha mabomu ya machozi kurudi nyuma na kile cha silaha za moto.

Kadhalika alidai kuwa kitendo cha washtakiwa kukiuka amri yake kupitia redio upepo iliyowataka kusitisha maandamano kwa mara ya pili, alilazimika kuamuru askari wenye silaha ya moto kusonga mbele.

SSP Rich ambaye pia ni Ofisa wa Polisi wa Operesheni Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, alitoa ushahidi wake jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, anayesikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimba, akisaidiana na Mawakili wa Serikali, Wankyo Simon, Jacqline Nyantori na Salim Msemo.

Akiongozwa na Nchimbi shahidi alidai kuwa Februari 16, 2018, aliitwa na bosi wake Kamanda wa Poli... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More